Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA- Siku hii ya Ashura ni lazima ikumbukwe kila siku na kila saa kwani mambo walofanyiwa familia ya Mtume(saw) ni mambo hayastahamiliki, kuuawa Hussein(as) ni pigo kwa Umma wa Kiislam.
Hivi kwa nini kuna watu wanaopinga kifo cha Imam Hussein (as)?! Na kwa nini baadhi ya Waislam wajitahidi kuficha siku adhimu kama hii kuwambia watu kua Mashia ni makafiri kwa sababu ya kuadhimisha kifo cha mjukuu wa Mtume(saw).
Siku hii itaadhimshwa na kuendelezwa na kuelezea kilichotokea ndani ya ili watakaokuja baada yetu wajuwe nini kilicho msibu mjukuu wa Mtume Muhammad(saw).